Amir-Abdollahian aliyasema hayo katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Uingereza David Cameron jana Jumapili, walipojadili uhusiano wa pande mbili na matukio ya hivi karibuni ya kikanda.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran amesema kwamba chanzo cha mgogoro wa Palestina kinarudi nyuma hadi miaka 75 ya kukaliwa kwa mabavu ardhi za Wapalestina na Israel, kuendelea kukiukwa haki za kimsingi za Wapalestina, na jinai za kivita zinazofanywa katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu ambapo nafasi ya Uingereza katika masuala hayo iko wazi kabisa.
Aidha amelaani kimya cha baadhi ya serikali za Magharibi kuhusiana na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia huko Gaza katika kipindi cha siku 80 zilizopita na kusisitiza kuwa, harakati ya muqawama wa Palestina Hamas ni harakati ya ukombozi dhidi ya uvamizi na utawala wa kibaguzi kama ilivyokuwa huko Afrika Kusini kwa miaka mingi.Amir-Abdollahian ameelezwa matumaini yake kwamba Uingereza kwa kuchukua misimamo thabiti na inayofaa itasaidia kuboresha uhusiano wa kikanda na wa nchi mbili.
Kwa upande wake Cameron ametoa wito kwa Iran kufanya juhudi za kuzuia kuenea wigo wa vita katika eneo na kuimarisha usalama wa baharini.
Pande hizo mbili pia zimetoa wito wa kuendeleza mashauriano na kubadilishana mawazo juu masuala yenye maslahi ya pande mbili.Israel ilianzisha vita dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba baada ya Hamas kutekeleza Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya maeneo yanayokalia kwa mabavu na vilevile kujibu dhulma ya miongo kadhaa ya utawala wa Israel ya mauaji na uharibifu huko Palestina. Uchokozi huo wa Israel hadi sasa umepelekea kuuawa shahidi takriban Wapalestina 22,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Watu wengine 55,600 wamejeruhiwa huku miili mingi ikisalia chini ya vifusi. Utawala wa Tel Aviv umeweka mzingiro kamili katika eneo hilo, na kuzuia kuingia huko mafuta na kukata umeme, chakula na maji kwa Wapalestina zaidi ya milioni mbili wanaoishi katika Ukanda huo.
342/